1.Kutokwa na damu nyingi kupita kiasi Hapa mwanamke hutokwa na damu nyingi na kwa kasi kuliko kawaida na hubadilisha pedi au kitambaa mara kwa mara. Hapa jitahidi kumkumbusha mpenzi wako kuwa msafi zaidi, pia mpe vyakula na matunda yenye madini ya chuma ili kuongeza damu mwilini 2.Siku zinazobadilika Hii hutokea pale mwanamke anapopata siku zake mapema au kuchelewa hivyo kutokutambua tarehe maalumu. Hapa jitahidi kufuatilia tarehe za mpenzi wako vizuri na kumkumbusha kuwa makini, pindi muda unapokaribia. 3.Maumivu makali wakati wa hedhi Hii husababishwa na kusinyaa na kutanuka kwa ukuta wa mimba ambao hutolewa sambamba na damu inayotoka. Hapa jitahidi kumtuliza na kumliwaza mpenzi wako kwa kumkanda na kitambaa chenye maji ya vuguvugu maeneo ya tumboni mwake kwa taratibu zaidi kupunguza maumivu, pia yakizidi sana mshauri kwenda kwa daktari au kutumia...
The real purpose of Life