Skip to main content

FAHAMU SIRI MUHIMU KUKUWEZESHA KUFIKIA MAFANIKIO YAKO KIUCHUMU

Tupo kwenye ulimwengu wa karne ya 21, ambao kila kitu kinahitaji gharama za pesa, Ukiwa unahitaji familia, mke, watoto, biashara, matibabu, nyumba, gari, n.k basi huna budi uwe na pesa ili ikuwezeshe kumudu gharama hizo.

Mafanikio kiuchumi yanahitaji mtu anaejielewa vizuri, na zifuatazo ni SIRI kubwa ambazo zitakuwezesha kujikwamua kiuchumi;

1.Akili ya Biashara; ndiyo siri kubwa katika mafanikio yako kiuchumi ni akili yako kibiashara, Siku zote wanaofanikiwa kiuchumi ni wale wenye uwezo wa kutumia fedha ndogo ili kuzalisha kiasi kikubwa.Jaribu kuweka akiba ili uwekeze kuliko kutumia fedha nyingi kwa starehe.

2.Kuweka akiba, itakayokuwezesha kuwekeza.

3.Kufanya kitu ambacho unakipenda. Kumbuka siyo kila alichofanya mwenzako akafanikiwa ndio hicho na wewe ukifanya utafanikiwa. Fanya kitu kutoka moyoni na utafanikiwa zaidi.

4.Ubunifu. Ndio, kuwa mbunifu ndio silaha kubwa ya kufanikiwa kiuchumi.Fikiria njia tofauti ambayo itakutambulisha wewe, tofauti na wengine.

5.Uvumilivu na Kujiamini. Biashara yoyote inahitaji uvumilivu na ujasiri kwanza.

6.Omba ushauri kwa waliotangulia. Ndio ukitaka kufanikiwa kiuchumi, jenga tabia ya kuwa mdadisi na kuomba ushauri kwa waliofanikiwa katika kile unachokifanya.

7.Jenga tabia ya kusoma na kutizama vyombo vya habari kama, TV, kusikiliza Radio, na kusoma articles kwenye mitandao zinazohususu Uchumi.

Hii ni moja kati ya mtandao ambao siku zote utakupa habari za maisha Halisi na nini chakufanya kujikomboa Kiuchumi. Ungana nasi Facebook kwa kulike ukurasa wetu na Twitter ila upate taarifa hizi mara zinapotoka.Pia unaweza subscribe kwa email.

Mwisho, Jaribu kusoma Haya Maneno hapa chini yatakusaidia zaidi,




"Money will make you more of what you already are. If you're not a nice person, money’s going to make you a despicable individual. If you're a good person, money’s going to make you a better person." ~ Bob Proctor
"When I was young I used to think that money was the most important thing in life; now that I am old, I know it is." ~ Oscar Wilde
"It's good to have money and the things that money can buy, but it's good, too, to make sure you haven't lost the things that money can't buy." ~ George H. Lorimer
"The only way you can grow rich is by enriching others." ~ Matthias Schmelz
"Wealth is when small efforts produce big socioeconomic results which we can share. Poverty is when big efforts produce small socioeconomic results with nothing to share." ~ Firoz Shroff

"Set the bird's wings with gold and it will never again soar in the sky." ~ Rabindranath Tagore


Comments

  1. Kwa habari za uchumi na siri nyingi zaidi tembelea;
    http://www.bubblews.com/news/9053977-big-secretes-on-how-to-achieve-your-financial-success

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

AINA MBALIMBALI ZA JUICE ZA MATUNDA, NA FAIDA ZAKE KAMA DAWA MWILINI

Matunda ya asili ni tiba asilia. Pia mchanganyiko wa matunda haya asilia huweza kutengeneza juice tamu ambayo pia huweza kuwa tiba asilia. Zifuatazo ni baadhi ya Juice ambazo unaweza tengeneza wewe mwenyewe hapo nyumbani na zikawa ni kama tiba kwako; TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili. CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana. NANASI, APPLE NA TIKITIMAJI Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo. APPLE, TANGO NA ‘KIWI’ Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni ...

JUICE BORA ZA MATUNDA NA FAIDA ZAKE KATIKA KUBORESHA AFYA YA MWILI

Juisi ni kinywaji bora na maarufu duniani, lakini ni vyeme ukajua juisi ipi ina faida mwilini na ipi haina faida yoyote. Katika zama tulizonazo, kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa juisi, wakati si juisi bali ni vinywaji vyenye ladha ya matunda mbalimbali. Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia (preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki. Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini: KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO Juisi ya mch...

AINA ZA MATUNDA YENYE KUIMARISHA NA KUONGEZA MVUTO WA NGOZI YA MWILI

  APPLE: Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini tunda hili pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamini na madini kibao, pia lina kazi kubwa sana katika kukupa muonekano mzuri wa ngozi ya mwili wako.Tunda hili husaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kuhifadhi ngozi isipoteze uhalisia wake.   PAPAI: Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta, kurudishia au kuziba sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako. Papai pia hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na enzyme inayotokana papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka kutumia papai katika ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya na papai lililo iva na paka usoni kwako kwa dakika 10 kisha safisha, kisha utaona kitakachotokea katika uso wako, utaonekana kama ngozi ya mtoto wa siku mbili.   AVOCADO: Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juice, lakini huenda watu wakawa ha...