Skip to main content

FAHAMU JINSI YA KUFANIKIWA KIMAISHA

Kisaikolojia na kimaumbile binadamu wote ni sawa ila tunatofautiana jinsia na matumizi ya vitu tulivyopewa na mwenyezi Mungu. Na hii ndio hupelekea tofauti kubwa kati ya walichonacho (Matajiri) na wasionacho (maskini).

Katika kuanza na ulichonacho leo tunaangalia vitu sita ambavyo tumepewa kama zawadi na Mungu. Na kila mtu amepewa sawasawa na mwenzie ila tofauti ni matumizi yetu katika kutupatia kile tunachokitaka katika maisha yetu ambacho ni Mafanikio.

Ili kufanikiwa haijalishi upo katika hali gani, kitu kikubwa kwako ANZA NA ULICHONACHO KUPATA MAFANIKIO. Unaweza ukajiuliza kivipi? Usipate tabu. Ungana nami mzee wa Boda to Boda nikuhabarishe na kukupa nondo za kukuzindua katika usingizi ili upate mafanikio ya kweli.

1. AKILI.
Ni ukweli kila binadamu ana akili ya kung'amua jema na baya ila sio wote wanaojua thamani ya akili walizonazo. Wapo wanazitumia kwa faida na malengo na kupata mafanikio ila wapo wanaozitumia vibaya na kuishia kuishi maisha ya shida hadi wanakufa.

Ktk kuitumia akili ndipo huonekana tofauti ya wanaojua na wasiojua kitu. Wanaofuata mkumbo na wanatumia akili zao kufikiri na kuamua ni nini wafanye, kivipi na wakati gani. Ili kuonyesha matumizi sahihi ya akili kila binadamu anatakiwa kufikiri na kuwaza kabla ya kuamua kufanya jambo lolote katika maisha yake.

Ni vyema tusiwe watu wa kuamini kirahisi tunayoona na kusikia kwa watu na kuyafanya bila tafakari. Tuzitumie akili zetu katika kujituma na kufikiri kwa utofauti na wanavyofiki wengine . Tuwe tayari kujifunza kwa wenye elimu juu ya kile tunataka kufanya na sio kuiga wanavyofanya watu wengine.

2. MUDA.
Kila binadamu awaye yote ana muda na amepewa muda wa kuishi na kufanya mambo yake kwa  uhuru na amani . Lakini si watu wote wanaoutumia muda wao vizuri katika kujipatia mafanikio. Wengi hutumia ujana wao katika starehe, ulevi na kujirusha. Wengine wanatumia muda wao katika kufuatilia maisha ya watu kwa umbea na majivuno.

Pamoja na kutumia muda hovyo lakini kumbuka, huo ndio muda wako wa kujitafutia maisha na mafanikio. Muda ndio rasilimali muhimu kuliko zote ukiutumia vizuri hakika mafanikio utafanikiwa. Embu jiulize kuna tofauti gani kati ya tajiri na masikini katika muda? Kila mtu ana masaa  24 tofauti ni matumizi tu .

Ukafatilia utagundua, tajiri ana panga malengo na mipangilio yake katika siku wakati maskini hana mipangilio na muda wake anaweza kushinda asubuhi hadi jioni anaangalia  Tv au movie ambazo hazimsaidii kitu katika maisha yake. Jiangalie vizuri unatumiaje muda wako ili kuyafikia mafanikio yako?

3. WATU.
Kila mtu iwe kwa kutaka au kutotaka amezungukwa na jamii ya watu. Na kimsingi umepewa watu hao na Mungu ili uweze kuwatumia na kupata kile unachotaka. Kuna wale wa hiyari na ambao unalazimika kuwatafuta mwenyewe ili wakusaidie kupata kile unataka katika maisha yako.

Kwa  mfano mwalimu inabidi umtafute ili akupe elimu, wataalamu wa afya inakulazimu uwafuate ili wakutibu. Lakini kuna watu ambao umepewa bila kutaka au kupanga wewe kama wazazi na ndugu wengine. Hakuna aliyepanga kuzaliwa na wazazi fulani au kuzaliwa tumbo moja na mtu fulani bila kujali ni masikini au tajiri.

Lakini kutokana na watu hawa unaweza na unapaswa uwatumie katika ushauri na maarifa waliyonayo ili kupata kile unachotaka ambacho si kingine ni mafanikio. Kushindwa kwako kuwatumia watu hawa hili litakuwa ni tatizo lingine ambapo ukishindwa kufanikiwa usimlaumu mtu.

4. KIPAWA / KIPAJI.
Huu ni uwezo wa ndani alionao kila binadamu bila kujali kabila lake au rangi yake ama kile anachoweza kukifanya tofauti na wenzake. Hicho ndicho kipaji na mtu akikigundua na kukitumia vizuri hupata mafanikio kwa haraka.Tena ndio wale ambao muda mfupi hupata utajiri wa ghafla na watu kusema kajiunga na Freemason huyo au amemuua mama yake ili apate utajiri na maneno mengineyo.

Siku zote tafuta ukijue kipaji chako na kitumie upate utajiri na mafanikio katika maisha yako. Unapokuwa na kipaji na ukikitumia ipasavyo mafanikio makubwa yanakuwa upande wako. Jaribu kuangalia watu wote ambao walimudu kutumia vipaji vyao kwa namna moja au nyingine maisha yao yako vipi, bila shaka ni ya mafanikio makubwa sana.

5. NGUVU.
Kila mtu amepewa nguvu na uwezo wa kufanya jambo fulani.Tunaweza kuzitumia nguvu zetu katika kilimo, biashara na hata kazi yeyote halali na kujipatie kile tunataka katika maisha. Tatizo watu wengi tumebweteka tunataka maisha rahisi tulale tuamke kesho matajiri bila kufanya kazi.
Vijana wengi utakuta wanataka kufanya kazi rahisi na kupata faida kubwa.

6. AFYA.
Kila binadamu amepewa afya ya mwili kabla ya kufikwa na maradhi. Tunapaswa tujue uzima na afya ni majaaliwa ya mwenyezi Mungu hivyo tuzitumie vizuri afya zetu katika kupata kile tunataka katika maisha yetu. Afya ni kitu cha muhimu kukilinda na kukitumia vilivyo kwa faida ya maisha yetu.

Ili tufurahie maisha yetu lazima tujali afya zetu kwa kula vyakula bora na vinywaji bora. Na sio kula ilimradi chakula.  Na kunywa ilimradi tu au kwa kuwa watu wanakula nasi tule. Tujitahidi kuzilinda na kuzitumia vizuri afya zetu ili tuweze kutimiza malengo.
Bila afya nzuri hakuna Mafanikio. Kila mtu na azingatie mbinu hizi ktk mafanikio yake zitamsaidia na kumwongoza.

Kabla ya kuhitimisha makala hii ni vyema ukajiuliza je, unatumia vizuri akili, watu, muda, nguvu, afya na kipawa ulichonacho kukusaidia kufikia mafanikio yako? Tafakari juu ya hili na chukua hatua.

Tutaendelea na mafunzo zaidi, hapa ndani

Comments

Popular posts from this blog

AINA MBALIMBALI ZA JUICE ZA MATUNDA, NA FAIDA ZAKE KAMA DAWA MWILINI

Matunda ya asili ni tiba asilia. Pia mchanganyiko wa matunda haya asilia huweza kutengeneza juice tamu ambayo pia huweza kuwa tiba asilia. Zifuatazo ni baadhi ya Juice ambazo unaweza tengeneza wewe mwenyewe hapo nyumbani na zikawa ni kama tiba kwako; TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili. CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana. NANASI, APPLE NA TIKITIMAJI Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo. APPLE, TANGO NA ‘KIWI’ Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni ...

JUICE BORA ZA MATUNDA NA FAIDA ZAKE KATIKA KUBORESHA AFYA YA MWILI

Juisi ni kinywaji bora na maarufu duniani, lakini ni vyeme ukajua juisi ipi ina faida mwilini na ipi haina faida yoyote. Katika zama tulizonazo, kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa juisi, wakati si juisi bali ni vinywaji vyenye ladha ya matunda mbalimbali. Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia (preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki. Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini: KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO Juisi ya mch...

AINA ZA MATUNDA YENYE KUIMARISHA NA KUONGEZA MVUTO WA NGOZI YA MWILI

  APPLE: Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini tunda hili pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamini na madini kibao, pia lina kazi kubwa sana katika kukupa muonekano mzuri wa ngozi ya mwili wako.Tunda hili husaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kuhifadhi ngozi isipoteze uhalisia wake.   PAPAI: Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta, kurudishia au kuziba sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako. Papai pia hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na enzyme inayotokana papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka kutumia papai katika ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya na papai lililo iva na paka usoni kwako kwa dakika 10 kisha safisha, kisha utaona kitakachotokea katika uso wako, utaonekana kama ngozi ya mtoto wa siku mbili.   AVOCADO: Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juice, lakini huenda watu wakawa ha...