*MADHARA YA ZINAA KISAYANSI*
Wengi katika wanadamu wanajaribu kuhoji kwa nini Allah anakataza zinaa wakati kuingiliana baina ya mke na
mume na kuingiliana baina ya hawara na hawara mambo ni yale
yale, sasa kwa nini akataze???
Kwanza ifahamike kwamba Allah akikataza jambo
basi ujue lina hasara kwetu kwa kulifuata na lina faida kubwa kama
tukiliacha. Tofauti na wanadamu, kwa mfano; Serikali inakataza pombe ya Gongo kwa madai kuwa ni haramu wakati Bia pia ni pombe lakini ni halali! Hiyo ni kwa mujibu
wa serikali za ulimwengu. Lakini
katika UISLAMU Mwenyezi Mungu
akisema pombe ni haramu basi iwe Gongo,Bia,n.k zote ni HARAMU.
Ndivyo pia ilivyo ZINAA, leo ulimwenguni kuna zinaa ya halali
wenyewe wanaita “zinaa salama ya kutumia Condom” lakini uislamu
umeharamisha kabisa zinaa, iwe ya Condom au bila Condom huo
ndio uislamu na ndiyo amri za Allah.
Allah anasema katika
Qur’an, sura ya 17 Bani Israil aya ya 32;
"Na wala msiikaribie ZINAA, hakika ya hiyo zinaa ni uchafu na njia
mbaya"
Hapo allah amekataza
Zinaa, tena amesema hiyo zinaa ni uchafu. Haya ni maneno aliyosema
Allah katika karne ya saba (7).
Je? Watu wa kanuni za maumbile wanakubaliana kwamba ndani ya
zinaa kuna uchafu? Na kama upo ni upi? Hatuwezi kuujua uchafu wa zinaa mpaka tutazame katika mafundisho ya wanasayansi wa
sasa yaani *MODERN SCIENTISTS* ili
tujue wamekubaliana vipi na Qur’an bila wenyewe kujua. Wakati tunatafuta kujua uchafu wa zinaa
na madhara yake kisayansi lazima
kwanza tujue vitu vikuu vine:
(1) *Uchafu ni nini?*
(2) *Manii yanatoka wapi kwa mwanaume*
(3) *Manii yanatoka wapi kwa mwanamke.*
(4) *Na ndani ya manii mna nini.*
Tunapozungumzia uchafu kwa tafsiri ya jumla ni kitu kilichowekwa mahala pasipostahili.
Mfano; kuchukua kiatu chenye thamani ya laki moja ukakanyaga
matope kisha kiatu kile ukakiweka juu ya kitanda cha kawaida na godoro la sufi ambacho thamani
yake kwa ujumla havifiki elfu arobaini; lakini pamoja na thamani ya kiatu kuwa kubwa kuliko kitanda na godoro mtu akija
atauliza huu uchafu aliyeweka hapa juu ya kitanda ni nani? Kwa
nini aite kiatu cha gharama uchafu? Ni kwamba kimekaa
pahala pasipostahili. Hivyo kitendo cha mwanaume au mwanamke kupokea au kupeleka manii yake pahala pasipokuwa halali yake huo ni uchafu.
Kwa upande wa mwanaume
tunapozungumzia utoaji wake wa manii ni mfinyo wa glands (tezi) za aina tano; ambao mfinyo huu
unapatikana baada ya mwanaumekupata stimulation (msisimko) na hapo ndipo tezi hizi hujibinya na kutoa maji ya aina tano tofauti yanayokutana katika makende na
kuchukua mbegu kisha yanatoka katika hali na rangi ambayo wengi
tunaifahamu. Glands hizi za mwanaume zimefungwa baina ya
kifua na mgogo.
Kwa mwanamke manii yake yanatoka katika Glands za aina mbili tu ambazo hizi zimefungwa
katika kifua chake. Hivyo maji haya
yanayotoka katika glands hizi mbili
yakichanganyika na ya mwanaume jumla yanakuwa maji ya aina saba (7) yakikaa katika pahala
panapokusudiwa kwa mwanamke na kwa muda maalum hapo ndipo inapopatikana mimba na kizazi cha
binadamu kinaendelea.
Baada ya kujua hatua ya mwanzo yanapotokea manii sasa tuingie katika hatua ya pili ya kujua je?
Ndani ya manii mna kitu gani kitaalamu. Ndani ya manii mna vituvikuu vine:
• *PROTEIN*
• *ACID*
• *SPERM/CHROMOSOME*
• *VIRUS*
*PROTEIN:* Ni aina mojawapo ya
“Food Substance” inayorutubisha
mwili. Substance hii inapatikana ndani ya manii na pia watu wa
mambo ya reproduction system
(mfumo wa uzazi) wanakubali kwamba manii yanatokana na aina hii ya chakula na ndiyo maana kama una njaa shughuli ya Jimai inashindikana, au kama utajilazimisha utapata madhara.
*ACID:* Ni mfano wa tindikali, yaani
kitu chenye ladha ya ukali mfano ndimu. Na kitu chenye tindikali
kina kawaida ya kuunguza na pia
kulegeza kwa itakayompata au
kumuingia, ndiyo sababu kitaalam
ukimlinganisha mwanamke aliyeolewa na asiyeolewa kisha
akawa hafanyi zinaa maumbile yao
yanatofautiana. Yule aliyeolewa mwili wake unakuwa laini zaidi
sababu ya acid inayopatikana ndani ya manii. Nitakupa mifano mingi iliyo hai ili akili yako ikubali
kwamba vyote vinavyotajwa vinapatikana ndani ya manii.
Ukitaka kuthibitisha zaidi acid ya katika manii ambayo inaunguza nakulegeza hata ukiwa na kidonda
kibichi ukitia manii kitauma mara mbili zaidi sababu ya acid. Mfano mwingine tazama kwa wale
watoto wa kiume ambao wanaingiliwa kinyume na maumbile (mashoga) hata kama
zamani alikuwa strong (imara) kiasi gani akiingiliwa tu, basi
analegea kuanzia kutembea, kuzungumza na kila kitu sababu ni Acid inayopatikana ndani ya manii.
Pia ndio maana inakatazwa kumuingilia mwanamke
anayenyonyesha sababu
ukimuingilia ukamuingizia manii
ambayo yana acid, acid ile itapanda
katika maziwa na kuyaharibu maziwa na hapo mtoto akinyonya
atanyonya maziwa yenye acid.
Itasababisha mtoto kulegea au kwa watu wa pwani wanaita
kubemendwa, hivyo mtakua mmemharibu mtoto. Lakini kama
atakula acid ya baba yake hatadhurika sana, sababu atakula acid ambayo kwa asili ndiyo iliyomtengeneza. Ila mkeo akiziniwa na mtu mwingine mtoto
ataathirika sana na pengine itakuwa ni sababu ya kifo chake
kwa kuwa amekula acid ambayo si ya asili kutoka kwa wazazi wake hivyo itakuwa ni POISON (sumu)
kwake. Kazi kubwa ya acid kwenye manii ni kuua bacteria zisizohusika zinazopatikana wakati zikitoka kuelekea katika virginal wall.
SPERM: Ni mbegu za kiume zinazopatikana ndani ya manii na
hizi mbegu haziishi ndani ya mwili kwa sababu ya hali ya joto la mwili, kwani mtu wa kawaida ambaye
haumwi anakuwa na nyuzi joto 37 hivyo mbegu zitakufa kutokana na joto la ziada. Wataalamu wa
mambo ya reproduction na
gynecology wanatueleza kwamba
mshindo mmoja una wastani wa watoto milioni 200 hadi 300.
Lakini yanayofanikiwa kulifikia yai ni mia moja tu. Na yanayofanikiwa
kuingia kwa kawaida ni moja au mawili yakizidi sana manne tu, na si zaidi ya hapo, lau kama yakizidi
basi ni kwa miujiza yake Allah.
VIRUS: Hivi ni vijidudu ambavyo kila
mtu anavyo vya kwake na pia haviingiliani baina ya mtu na mtu
na hapa ndipo tutaeleza kwa kina
madhara ya zinaa kisayansi. Lazima
pia tujue kuwa Virus wanafanya kazi gani na pia wanakwenda
wapi. Katika virginal wall kuna vijistomata (vitundu) maalum kwa
ajili ya kupokea virus; sababu mwanaume anapotoa manii yake
yenye protein, acid, sperm/chromosomes na virus kila kimoja
huchukua nafasi yake kwenda kunapohusika. Nafasi ya virus ni
kuingia katika vitundu vilivyo katika virginal wall ili vipate kuishi
humo kwa kuwa ndipo
alipowapangia Allah.
Hivyo basi ukiwa unamuingilia mkeo na ukitoa manii basi moja
kwa moja virus wako watakwenda kuingia katika vijitundu vilivyo
kwenye virginal wall ili kuishi humo. Ina maana virus watakaoingia kuishi kwa mkeo ni wale ambao wamezoeana. Sasa ikija kutokea mkeo akazini na
mwanaume mwingine ataingiziwa virus wasiokuwa wako. Hivyo hawa wapya wakiingia nao pia
watataka kuingia katika yale matundu ili nao wakaishi. Kwa
kuwa ndivyo alivyowapangia
Allah, hawa wapya
wakiingia tu wale wa zamani ambao ni wa mume, watawashangaa, watajiuliza hawa
nao wametokea wapi? Mbona si katika wale tuliozoeana? Kwa
kushangaa huku wale virus wenyeji watawashambulia virus wageni kama antibody bacteria
(kitu kinachotoka nje ya mwili). Na katika mapigano haya watapelekea
kundi moja kufa na kundi moja likifa lazima wale waliokufa
watoke, watatoka vipi? Au watatokea wapi? Jibu ni pale pale
walipoingilia. Hapo sasa ndipo mtu anapoanza kutokwa uchafu. Na pia
virus wapya waliosalimika
wakiona wanazidi kushambuliwa
na virus wa zamani itabidiwatoboe sehemu nyingine
zisizohusika ili wakimbie na kujificha katika nyama laini.
Hapo ndipo mtu anapoanza kupata
maumivu makali wakati wa kukojoa na pia ndio chanzo cha
magonjwa mbalimbali ya zinaa, nawakati huo mume akimuingilia
mkewe naye pia atapata ugonjwa
wa zinaa sababu atakutana na virus wageni waliojificha kujihami katika sehemu laini zisizohusika
watamuingia mume kupitia mrija wa urinary truck (mrija wa mkojo).
Ndio sababu Allah
akasema zinaa ni uchafu. Na uchafu unaokusudiwa ni
kuchanganya mifumo tofauti ya mwili yaani mwanamke kuingiliwa
na mwanaume zaidi ya mumewe pekee. Na hapa ndipo tunapoona
hekima ya Allah
kwamba kwa nini ameamrisha mwanamke kuolewa na mwanaume mmoja na mwanaume
kuoa mwanamke zaidi ya mmoja.
Hii ni kwa sababu mwanamke anapokea manii yenye kubeba
VIRUS wa asili kutoka kwa mumewe. Hapa ndipo inapopatikana hekima ya ya
mwanamke aliyefiwa na mumewe au aleyeachwa kwa talaka lazima akae eda. Eda si tu kuangalia kama
mwanamke ana mimba, bali pia
katika kipindi cha miezi mine na siku kumi ambacho mwanamke
anakaa eda kwa kuwa katika kipindi hicho haingiliwi ina maana
wale virus watakosa protein inayopatikana katika manii ambayo ndio chakula chao, hivyo kwa kukosa chakula watakufa.
Kwa hiyo katika kipindi hicho mwanamke anaandaliwa ili kama
ataolewa tena na mume mwingine
huyu mume mpya ajitengenezee mifumo yake mipya ambayo
haitapingana na ile ya mwanzo.
Hivyo Allah alipokataza ZINAA anajua kwa kina madhara yake.
Ndio sababu twasema kwamba sera bora za kupambana na
magonjwa mbalimbali ya zinaa kama UKIMWI n.k dunia nzima ni kufuata UISLAM tu hakuna la zaidi.
Hivyo tunapenda watu walifahamu hilo na kulifanyia kazi kwa kuwa UISLAM siyo ugaidi wala si dini ya
vurugu bali ni dini ya AMANI ambayo inaweza kumfaa mtu
kimwili na kiroho. Tunatoa wito kwa watu ulimwenguni kote
kumuamini Mwenyezi Mungu wa kweli na Mtume wake wa karne ya sayansi na teknolojia Nabii
Muhammad صلى الله عليه وسلم ili kupata nusra
ya mitihani mizito na majanga yanayotukumba wanadamu hivi
sasa.
Matunda ya asili ni tiba asilia. Pia mchanganyiko wa matunda haya asilia huweza kutengeneza juice tamu ambayo pia huweza kuwa tiba asilia. Zifuatazo ni baadhi ya Juice ambazo unaweza tengeneza wewe mwenyewe hapo nyumbani na zikawa ni kama tiba kwako; TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili. CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana. NANASI, APPLE NA TIKITIMAJI Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo. APPLE, TANGO NA ‘KIWI’ Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni ...
Comments
Post a Comment