Skip to main content

MAMBO AMBAYO KIJANA HUTAKIWI KUYAFANYA…

(1). Kuchagua Kazi.

Ni vigumu kupata Kazi ukiwa nje ya Kazi. Fanya Kazi uliyoipata upate Kazi unayoitaka.

(2). Kuchagua sehemu ya kuishi /kufanyia Kazi.

Maisha ni safari ndefu, maisha ni popote, si lazima kukaa mjini. Hauwezi kujua ni sehemu gan iliyobeba mafanikio yako. Chagua sehemu yenye FURSA na si yenye  MAGHOROFA.

(3). Kuishi bila kuwa na malengo.

Maisha si bahat mbaya au nzuri. Maisha ni mipango, Maisha yanaongozwa na malengo. Vile ulivyo leo ni matokeo ya jinsi  ulivyopanga jana, na vile unavyoishi leo ndivyo kesho yako itakavyokuwa. PANGA KESHO YAKO SASA.

(4). Maisha Ya kuiga.

Maisha yako si ya mwenzako, na ya maisha ya mwenzako si ya kwako. Si kila ukionacho ni lazima ufanye, chagua kipi cha kufanya na kipi cha kuacha. Kupitwa na jambo wakat mwingine sio USHAMBA ni BUSARA.

(5). Kuishi juu ya kipato chako.

Ishi kulingana na vile ulivyonavyo na si usivyonavyo. Kuwa na Busara katika MATUMIZI uepukane na MADENI yasiyo na ULAZIMA. RIDHIKA NA VILE ULIVYONAVYO.

(6).Kuishi bila AKIBA.

kuweka akiba ni TABIA sio kiwango kikubwa cha Pesa. Jenga tabia ya kujiwekea akiba. Haujui ni kipi kitakupata muda USIOTEGEMEA.

(7). Kuishi kwa kutegemea MSHAHARA.

Mshahara haujawahi kutosha na hautatosha kama ukishindwa kuishi chini ya kipato chako  na kuwa na njia mbadala za kuinua kipato chako. JARIBU NJIA ZINGINE MBALI NA MSHAHARA.

(8).Kushindwa Kupangilia MATUMIZI ya Pesa.

Maamuzi yako ya pesa ndiyo yatajayoamua hali yako ya kiuchumi baadaye. Ni muhimu kujua kipi cha kununua, kwa wakat gani na kwa sababu gani. Jifunze kutofautisha kati ya liability (dhima) mfano: gari ya kutembelea na assets (kitegauchumi) mfano:nyumba au kiwanja . TUMIA PESA YAKO KUNUNUA ASSETS KULIKO LIABILITY.

(9).Kushindwa kutumia MUDA wako VIZURI.

Changamoto kubwa inayotukabili vijana ni kushindwa kujua namna ya kutumia vizuri muda. Tumia muda wako mwingi kujiendeleza ufahamu wako kwa kujisomea, kupanga malengo yako ya maisha, kujiuliza ni wapi ulikosea na nini ufanye ili urekebishe hayo makosa na muda mchache ufanye wa mapumziko na kufanya vitu vya kufurahisha akili yako kama kuangalia movie, mpira, kuingia kwenye mitandao ya kijamii Facebook, watsap n. k. Kumbuka muda ni rasilimali isiyoweza kurudishwa pindi unapopotea.

(10).Kuoa bila ya kujipanga kimaisha. (premature marriage).

Hii inawahusu wanaume, swala la kuoa ni pana sana na kila mtu ana vigezo vyake na mtazamo wake kufanikisha jambo hilo. Ila jambo la msingi ni hili, jiandae kwanza kiuchumi kabla hujaingiza majukumu mengine, unapoa ujue umekubali kusaidia upande wa mwanamke, upande wa familia yenu bila kusahau familia yako binafsi. Hata kama maisha ni kusaidiana na huyo utakayemuoa ila nafas yako kama mwanaume ITABAKI pale Pale. JIPANGE KWANZA.

MWISHO : UJANA NI KIPINDI AMBACHO NAKIFANANISHA NA KAMA SHAMBA LENYE UDONGO MZURI LINALOPOKEA KILA AINA YA MBEGU.. SASA ITATEGEMEA UNAPANDA NINI..!

*****Panda Chema Uvune Mema ***
Have a nice day my friends

Comments

Popular posts from this blog

AINA MBALIMBALI ZA JUICE ZA MATUNDA, NA FAIDA ZAKE KAMA DAWA MWILINI

Matunda ya asili ni tiba asilia. Pia mchanganyiko wa matunda haya asilia huweza kutengeneza juice tamu ambayo pia huweza kuwa tiba asilia. Zifuatazo ni baadhi ya Juice ambazo unaweza tengeneza wewe mwenyewe hapo nyumbani na zikawa ni kama tiba kwako; TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili. CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana. NANASI, APPLE NA TIKITIMAJI Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo. APPLE, TANGO NA ‘KIWI’ Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni ...

JUICE BORA ZA MATUNDA NA FAIDA ZAKE KATIKA KUBORESHA AFYA YA MWILI

Juisi ni kinywaji bora na maarufu duniani, lakini ni vyeme ukajua juisi ipi ina faida mwilini na ipi haina faida yoyote. Katika zama tulizonazo, kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa juisi, wakati si juisi bali ni vinywaji vyenye ladha ya matunda mbalimbali. Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia (preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki. Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini: KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO Juisi ya mch...

AINA ZA MATUNDA YENYE KUIMARISHA NA KUONGEZA MVUTO WA NGOZI YA MWILI

  APPLE: Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini tunda hili pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamini na madini kibao, pia lina kazi kubwa sana katika kukupa muonekano mzuri wa ngozi ya mwili wako.Tunda hili husaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kuhifadhi ngozi isipoteze uhalisia wake.   PAPAI: Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta, kurudishia au kuziba sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako. Papai pia hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na enzyme inayotokana papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka kutumia papai katika ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya na papai lililo iva na paka usoni kwako kwa dakika 10 kisha safisha, kisha utaona kitakachotokea katika uso wako, utaonekana kama ngozi ya mtoto wa siku mbili.   AVOCADO: Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juice, lakini huenda watu wakawa ha...