Skip to main content

SIRI KUBWA KUFANIKIWA MAISHA KABLA YA MIAKA 40

Kuna makundi manne (4) ya watu wanaotengeneza pesa hapa duniani.

1. WAAJIRIWA.
Hawa ni watu ambao kimsingi wanauza muda wao almost wote wa siku nzima kwa mwajiri wao na yeye anawalipa pesa kwa kuwaambia cha kumfanyia. Kwa kuwa kanuni ya mshahara huwa ni kumlipa mtu 10% ya anachozalisha hasa kwa makampuni makubwa basi haitakaa itokee mwajiriwa kulingana kipato na mwajiri wake. Na hivyo wengi wa waajiriwa hufa #maskini na watoto wao pia kuanza kutafuta maisha kivyaovyao kwa kusoma na kuja #kuajiriwa pia hivyo hivyo..
Usikubali kubaki kwenye ajira unalipwa laki 5 kwa mwezi sawa na Tsh 1,850 yaani chini ya dola moja kwa saa. Ina maana umesoma mpaka chuo kikuu halafu thamani ya lisaa lako moja ni less than $1!!!!? Ndiyo maana watu wengi waliosoma sana huwa hawawezi kuwa matajiri kwa sababu wanauza muda wao kwa "bei chee" halafu siku zinazidi kuyoyoma haoni mafanikio. Huku tena ana mkopo wa gari nk. Makato na marejesho... Kwa nini usife masikini kwa style hiyo.?

2. WALIOJIAJIRI
Hawa hujitambua kidogo na kuamua kufanya kazi binafsi au kufungua biashara ndogo kama duka nk. Lakini kwa kuwa hawana pesa ya kununua muda wa watu wengine na kuwaajiri hawa nao huwa busy kutwa kucha bila mafanikio ya maana. Ana duka miaka 15 sasa halijawahi kupanuka likawa supermarket. Na mara nyingi huyu mtu akifa na biashara yake nayo humfuata. Ndo watu wanasingizia eti alikuwa na biashara za "uchawi". Kumbe shida ni kuwa kila kitu kilikuwa kinamtegemea yeye.

3. WAMILIKI WA BIASHARA KUBWA
Hawa huwa na kipato endelevu (residual income) maana amemunua muda wa watu weeengi kawaajiri halafu kawapa majukumu kwa hiyo awepo asiwepo pesa inaendelea kuingia kwake. Mfano kina Bakhressa, Mengi, Dewji, etc. Majina yao yanajulikana. Ni wachache nchi hii. Ukihesabu vidole vyako vya mikono na miguu majina yataisha kabla hujamaliza kuhesabu.

4. WAWEKEZAJI
Hawa ni watu wenye pesa nyingi zaidi na wana uwezo wa kuiwekeza mahali hata nje ya nchi ikawa inawazalishia pesa zaidi bila wao kuwepo kabisa. Hawa hata majina huwa  hawajulikani

Kwa hiyo nadhani tayari wewe unajua kundi lipi upo (ama kama wewe ni mwanafunzi unaweza kuona kundi lipi unaelekea).

SASA SIKIA...
Makundi mawili ya kwanza ni makundi ya watu maskini. Mfano waajiriwa ni watu wanaotumia muda wao na nguvu na maarifa yao yote (waliyoyakusanya kwa miaka mingi ya kusoma kwa shidashida) kumtajirisha mtu kwa malipo kidogo yanayomwezesha huyu muajiriwa kulipa kodi (siyo kujenga), kula, kuvaa,  kusafiri kwenda na kurudi kazini nk. Yaani basic needs tu. Maisha ya waajiriwa wengi yanafanana. Mfano ni wachache sana katika ajira ambao wamejenga nyumba zao binafsi kwa hela halali ya ajira. Kama vile ilivyo vigumu kwa mwanafunzi kwenda chuo kwa gari lake mwenyewe alilonunua kwa pesa yake halali. Wapo wachache sana. Na hivyohivyo waajiriwa kumiliki nyumba. Wengi wamepanga. Jiulize lini utafikia hizi level especially kama utang'ang'ania ajira tu bila kujishughulisha na kitu kingine cha ziada mpaka uzeeni? Ndo unastaafu unapewa kiinua mgongo lakini miaka 7 tu baada ya hapo unakufa kwa pressure. Coz ndo unaanza kuona wengine wa umri sawa na wewe wako mbaaaali kimaisha hapo nguvu za kuhimili mikikimikiki ya biashara huna tena watoto na wajukuu hawana future unaanza kupata stress. Kisa ulikuwa ungependa kiyoyozi cha kazini. Haya, endelea kufurahia kiyoyozi ndugu. Halafu mi huwa nashangaa..yaani unajua kabisa hapo kazini kuanzia kiti, dawati, computer, kalamu, karatasi, kula kitu si cha kwako. You are just hired to use them to produce for someone else. Hebu tufunguane macho leo..

Waliojiajiri nao wako busy. Kama ana duka basi kufata mzigo yeye (hamwamini mtu), kuuza yeye, usafi yeye, kuhesabu stock yeye, ulinzi wa duka yeye ndo analinda maana analala humo humo. Kama jongoo alivyo na miguu mingi lakini spidi "kiduchu" ndivyo na huyu nae. Miguu mingi ya jongoo bila macho is equal to ZERO. Na hivyo hivyo shughuli nyingi bila maarifa is uqual to ZERO. Yaani yuko busy kila saa lakini spidi ya mafanikio ni ndogo kweli kweli. Sasa maendeleo hayaji kwa style hiyo ila kwa kuwa hajui anahisi siku moja na yeye atakuwa kama Bakhressa. Kwani Bakhressa ndo anauza ice cream za Azam? Hujiulizi?

KWA WANAFUNZI..
Bahati mbaya sana kama ni mwanafunzi uko sekondari au chuo hiyo ndo ramani ya future yako.  Fikiria sasa itakuwaje.

HATA HIVYO.. kuna njia ya kukusaidia kuweza kuhama kutoka makundi hayo mawili kwanza na kuingia makundi mawili ya mwisho hapo juu.
Cha msingi ni Wewe kujishusha tu na kukubali  kuwa unahitaji kujifunza hivi vitu. Lakini ukifikiri kuwa unajua kila kitu kuna maarifa utayakosa simply kwa kutothamini mawazo ya wengine ambao huenda ni Mungu tu anawaleta ili kukustua kidogo upate ufahamu fulani. Kama umeajiriwa na unasoma ujumbe huu hebu jiulize ajira yako ikiisha leo ghafla PAAP!! Utaanzia wapi? Kama utaandika CV tena basi kubaliana na hali halisi tu kuwa wewe ni maskini. Huna cha kuuza kupata pesa zaidi ya muda wako. Kumbuka rasilimali ambayo Mungu aliwagawia wanadamu wote sawa ni MUDA. 24 hours kwa kila binadamu. Matajiri wananunua muda wewe unauuza. Yaani unafanya opposite na wanachofanya matajiri halafu unasema unataka kuwa kama wao. Unanielewa? Kuna mtu maarufu duniani anaitwa William Gates III au kwa jina maarufu Bill Gates, anasema, "KAMA ULIZALIWA MASKINI HILO SIYO KOSA LAKO ILA UKIFA MASKINI HILO NI KOSA LAKO". Jifunze.

Kuna tajiri mwingine anaitwa JACK MA huyu ni mmiliki wa ALIBABA. Yeye anasema hatua kuja duniani kufanya kazi tu mpaka siku ya kuta bali tulikuja kuishi maisha yetu. Anasema kuifanya kazi tu mpaka mwisho wa maisha yako utakuwa hujawahi kuishi maisha yako. Anasema siri ya mafanikio ni kutafuta kazi ambayo utaifanya kwa miaka mitano Kisha iwe imekupa pesa za kuishi maisha yako. Tafuta mpaka upiate. Kama hujaipata tafuta tu. Kama bado hujaipata watafute waliokwishaipata.
Unaona mawazo hayo?

Na kama wewe ni mwanafunzi hii ni habari njema sana maana ukiamua kujifunza vitu hivi sasa hivi ukavifanyia kazi, then I assure you miaka miwili au mitatu mbeleni wakati wenzako wanasambaza CV kuomba ridhaa ya kuingia kundi la kwanza la umaskini wewe utakuwa unanunua gari lako la pili au hata kiwanja na huenda umeanza kujenga kulingana tu na ndoto zako ni zipi.

Sababu zinaowafanya watu wengi kutofanikiwa ni pamoja na kupoteza muda mwingi kujadili vitu visivyo na tija maishani mwao hasa kwenye mitandao ya kijamii mfano sijui wimbo wa Snura, gari la Diamond, maisha ya Wema Sepetu, mambo mengi ya siasa ambayo kila siku ni mapya, matokeo ya mpira nk.

Katika kitu ambacho Mungu alitupa wote sawa ni muda. Jinsi Unavyotumia muda wako ndo inaamua hatma ya maisha yako.  Huwezi kufanikiwa maishani kama muda wako mwingi ni kujadili vitu visivyo na tija maishani mwako. Unasahau kuwa una mshahara mdogo haukutoshi hata kufanya chochote hilo ndo jambo la wewe kufikiria na kujadili.  Unaishi nyumba ya kupanga hujui lini utapata walau kiwanja uanze ujenzi nk. Una watoto au utakuwa nao siku moja wataishi kama watu au kwa kubahatisha bahatisha tu kama vile hukuwahi kuwatangulia duniani.  Ukiwaza haya mambo huwezi poteza muda kujadili Simba na Yanga au Sijui nani kapewa Wizara ya Mambo ya ndani.  Aisee. Time is money my friend.

Waingereza wanasema LIFE BEGINS AT 40. Yaani maisha huanza ukiwa na miaka 40. Kwa maana kwamba ukiwa na umri huo hutakiwi kuwa unawaza ada za watoto zinatakiwa ziwepo ulishatafutaga siku nyingi ukiwa na miaka 20-39. Wakati ukifika miaka 40 unapaswa uwe na nyumba gari urithi kwa familia yako biashara zilizosimama nk. Siyo ndo unaandika CV kuomba kazi ya tatu ili kuongeza kipato.
Life begins at 40.
How old are you?

Comments

Popular posts from this blog

AINA MBALIMBALI ZA JUICE ZA MATUNDA, NA FAIDA ZAKE KAMA DAWA MWILINI

Matunda ya asili ni tiba asilia. Pia mchanganyiko wa matunda haya asilia huweza kutengeneza juice tamu ambayo pia huweza kuwa tiba asilia. Zifuatazo ni baadhi ya Juice ambazo unaweza tengeneza wewe mwenyewe hapo nyumbani na zikawa ni kama tiba kwako; TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili. CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana. NANASI, APPLE NA TIKITIMAJI Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo. APPLE, TANGO NA ‘KIWI’ Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni ...

JUICE BORA ZA MATUNDA NA FAIDA ZAKE KATIKA KUBORESHA AFYA YA MWILI

Juisi ni kinywaji bora na maarufu duniani, lakini ni vyeme ukajua juisi ipi ina faida mwilini na ipi haina faida yoyote. Katika zama tulizonazo, kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa juisi, wakati si juisi bali ni vinywaji vyenye ladha ya matunda mbalimbali. Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia (preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki. Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini: KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO Juisi ya mch...

AINA ZA MATUNDA YENYE KUIMARISHA NA KUONGEZA MVUTO WA NGOZI YA MWILI

  APPLE: Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini tunda hili pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamini na madini kibao, pia lina kazi kubwa sana katika kukupa muonekano mzuri wa ngozi ya mwili wako.Tunda hili husaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kuhifadhi ngozi isipoteze uhalisia wake.   PAPAI: Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta, kurudishia au kuziba sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako. Papai pia hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na enzyme inayotokana papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka kutumia papai katika ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya na papai lililo iva na paka usoni kwako kwa dakika 10 kisha safisha, kisha utaona kitakachotokea katika uso wako, utaonekana kama ngozi ya mtoto wa siku mbili.   AVOCADO: Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juice, lakini huenda watu wakawa ha...