WAPENDAO NA WAPENDE
Aah!! Moyo nchi ya kiza,, wewe pofu waendaje??
Mji hisia fukiza,, mwenzangu umechotaje??
mimi zimenitatiza,, machozi yanitokaje??
MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE
Aah!! Nanena haya kwa ndani,, uwongo nitasemaje??
Utamu huo kinywani,, mapenzi umekaaje??
Niloipata tufani,, mapenzi yameumbwaje??
MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE
Dah!! moyo unanisimanga,, maumivu yakataje??
Haya hayana nyakanga,, mwalimu kaumiaje??
Shetani nyumba kapanga,, wazimu kaingiaje??
MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE
Doh!! sisemi naweka shonde,, waja mpate bwabwaje
nafsi yangu ni kibonde,, utamu ningepataje??
Mbio nakwepa makonde,, na nyie mlitakaje??
MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE
Dah!! Raha ya kuendeleza,, mwendo umepunguaje
japo nisema naweza,, mawazo nikapambaje
kumbe huitaji pweza,, mchuzi nitaunywaje
MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE
Duh!! Kukuru moyo kakara,, vuta vuta ngekujaje??
Mwili utake mitara,, nafsi nimechafukwaje??
Penzi sitaki hawara,, kukaa nitawezaje??
MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE
Dah!! Shavu limekuwa ziwa,, machozi yamekwamaje
Kwako nakiri pitiwa,, penzini nimekujaje??
Awali nilivutiwa,, makosa nimefanyaje
MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE
Dah!! Chozi lakujitakia,, kufuta linaumaje
Licha kukanywa tabia,, haraka nikaendaje
Kumbe moyo ni pazia,, wewe umelichanajeJ
MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE
Nuru ya penzi kuisha,, ahera imekaaje
sijapata kuridhisha,, nafsi yangu yajutaje
Kovu likija niisha,, salama niivaaje
MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE
najitenga nalo pendo,, kisiwa cha makengaje
Mana sijaona tendo,, furaha kunipataje
Si vyema kufata nyendo,, madhara yaniachaje
MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE
limetungwa na
HUSSEIN JAFARY JUMA
Comments
Post a Comment