Skip to main content

YAJUE HAYA UFANIKIWE KIUCHUMI

ACHA KUFANYA MAMBO HAYA NA UTAFANIKIWA 100%

1. ACHA KUWA NA MARAFIKI WANOKUPOTEZEA MUDA
Watu wengi tumekuwa na marafiki wengi sana na marafiki ni mhimu sana katika maisha yetu haya wapo wanaotufaa na wasiotufaa kuwa na marafiki wanao weza kukusaidia na kukupa hamasa ya kimaendeleo ,malengo yako na kuwa na maisha Fulani. Hivyo achana na marafiki wasio kuwa na msaada kwako.

2. ACHA KUKIMBIA MATATIZO YAKO
Waswahili wanasema kuwa “kukimbia tatizo si kutatua tatizo” Hivyo basi kama tatizo umekutananalo basi tafuta njia ya kulitatua tatizo hilo kwani matatizo hayaji kuisha katika dunia hii kama unakimbia utakimbia mangapi ? unatatizo la pesa kwanini usitafute pesa ila kama hufanyi kazi unategemea kupata pesa huwezi. Matatizo hayaepukiki komaa na ulitatue utajikuta kama uko peke yako katika hii dunia lakini kuna watu wana matatizo zaidi yako na wanahangaika kuyatatua.

3. ACHA KUJIDANGANYA MWENYEWE
Katika maisha ya sasahivi unaweza kumdanya mtu yoyote yule lakini ogopa sana kujidanganya. Vijana wengi tumekuwa tukijivuna mbele za watu kuwa tuna hili mara lile ili mradi tu tuonekane ni watu wazuri kwa watu wanao tusikiliza.

4. ACHA KUIGA MAISHA YA WATU WENGINE
Vijana wengi hili kwetu limekuwa janga kubwa sana maisha yetu yamekuwa yakuigiza sana (copy and paste) hasa hasa tunapenda kuonekana ni watu Fulani wenye maisha mazuri, hatuzijui shida ni watu wakula bata wakati si kweli. Maisha yetu yamekuwa magumu na yatakuwa magumu kwasababu ya kuiga maisha ya watu wengine ishi maisha harisi uliyonayo watu wakujua asili yako siyo kuigiza unaweza kosa kusaidiwa na watu.

5. ACHA KUKUMBUKA YALIYOPITA
Hapa kuna mambo mengi tunajifunza wengi hukumbuka yaliyopita hasa waliyo shindwa kuyafanya au yaliyowaumiza kwa kukumbuka yaliyopita haiwezi kukusaidia kwani kila tuamkapo asubuhi ni kama tumezaliwa upya na siku ni nyingine,tarehe na mambo utakayoyafanya ni mengine si sawa na jana. Waswahili wanasema “Tusahau yaliyopita tugange yajayo” hii ina maana kuwa wewe si wa kipindi kile bali ni mwingine na akili ni mpya.

6. ACHA KUOGOPA KUFANYA MAKOSA
Makosa ndiyo walimu wetu mkubwa sana katika maisha yetu na kila binadamu si mkamilifu toka uzaliwe mpaka sasa kuna makosa mengi uliyoyafanya na kupitia makosa hayo umejifunza kutorudia makosa tena na makosa hutujenga zaidi na kuwa makini zaidi kama ukifanya kosa huna haja ya kujilaum chukua muda kujilekebisha na kusonga mbele kosa lisiwe tatizo la kukukatisha tamaa.

7. ACHA KUNUNUA FURAHA
Vitu vingi tunavyo vihitaji vinagharama kubwa sana na vitu hivyo si kwamba tuna vipenda bali ni tamaa tu tuliyonayo na hiyo yote ni kuamini kuwa furaha ya maisha tutaipata huko si kweli. Mungu alitupatia furaha, na upendo bure ni vitu unavyozaliwa navyo fikiria kama vingekuwa vinauzwa wangapi? Wangapi tungekuwa hatuna furaha. Hivyo basi anza kuyafurahia maisha yako hivyo vingine vitakufuata.

8. ACHA KUSHINDANA NA MTU KIMAISHA
Acha kushindana na mtu kimaisha haitakusaidia huwezi jua yeye anafanya nini kuzipata pesa zake au mali zake na wewe unazipataje ushindani mzuri katika maisha ni ule wa kwako na mafanikio yako jiangalie kile unachokifanya na matokeo yake unapata nini? huo ndio ushindani mzuri kuliko wote sio kushindana na mtu kimaisha acha.

9. ACHA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO YASIYO SAHIHI
Katika mahusiano si kitu cha kujiingiza tu au kama unaoa si kuoa tu kwasabu Fulani kaoa basi na mimi nioe, si kudai kuwa nimechoka kufua ngoja nioe sasa ndiyo maana karne hii inaongoza kwa wanandoa kuachana na ndoa za utotoni kwasababu watu hawajipangi ni kuiga tu. Mahusiano au ndoa ni kitu kikubwa sana na kama umempenda mtu onyesha kuwa unampenda kweli mtangulize mbele yako kuwa ndiyo kila kitu kwako/ kila kitu kinaenda kwa ajiri yake. Kama unaingia katika mahusiano mheshimu mwenzako na kumpenda mpe nafasi kubwa katika maisha yako.

10. ACHA KUJILAUMU
Kuacha kujilaumu ni njia mojawapo ya kufanikiwa katiaka maisha yako unapo kosea amini kuwa wewe si mkamilifu na hakuna binadamu aliyekamilika jipange songa mbele. Wagunduzi wa vifaa mbalimbali vinavyotumika kama vya umeme na vinginevyo si kwamba hawa kufanya makosa walikosea sana mpaka kutoa kitu sahihi .

11. ACHA KUONGELEA YAWATU FULANI
Kuzungumzia maisha ya mtu Fulani haikusaidii ni kupoteza muda tu kwanini usiwaze maisha yako unatakiwa kufika wapi na ufanye nini kuishi maisha mazuri unakaa na kuanza kuzungumzia mtu Fulani yupo hivi mara hivi wakati huo huyo mtu unaemsema yeye yupo kazini we upo kijiweni mtalingana kweli? Acha kuzungumzia maisha ya watu fanya yako ufurahie maisha.

Comments

Popular posts from this blog

AINA MBALIMBALI ZA JUICE ZA MATUNDA, NA FAIDA ZAKE KAMA DAWA MWILINI

Matunda ya asili ni tiba asilia. Pia mchanganyiko wa matunda haya asilia huweza kutengeneza juice tamu ambayo pia huweza kuwa tiba asilia. Zifuatazo ni baadhi ya Juice ambazo unaweza tengeneza wewe mwenyewe hapo nyumbani na zikawa ni kama tiba kwako; TUFAHA NA TANGO LA KAWAIDA Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya huondoa harufu mbaya mdomoni na hupunguza joto la mwili. CHUNGWA, TANGAWIZI NA TANGO Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi na kuifanya kuwa laini. Pia hupunguza joto la mwili. Kwa wale wenye matatizo ya kuwa na ngozi kavu, juisi hii itawasaidia sana. NANASI, APPLE NA TIKITIMAJI Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hufanya kazi ya kuondoa chumvi nyingi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo na figo. Juisi hii ni nzuri kwa wale wenye matatizo ya kibofu na figo au wanaotaka kujikinga na magonjwa hayo. APPLE, TANGO NA ‘KIWI’ Juisi yenye mchanganyiko wa matunda haya hung’arisha rangi ya ngozi. Kiwi ni ...

JUICE BORA ZA MATUNDA NA FAIDA ZAKE KATIKA KUBORESHA AFYA YA MWILI

Juisi ni kinywaji bora na maarufu duniani, lakini ni vyeme ukajua juisi ipi ina faida mwilini na ipi haina faida yoyote. Katika zama tulizonazo, kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa juisi, wakati si juisi bali ni vinywaji vyenye ladha ya matunda mbalimbali. Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia (preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki. Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini: KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO Juisi ya mch...

AINA ZA MATUNDA YENYE KUIMARISHA NA KUONGEZA MVUTO WA NGOZI YA MWILI

  APPLE: Hili ni tunda maarufu sana duniani lihusishwalo na wapendanao, lakini tunda hili pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani na kuwa na vitamini na madini kibao, pia lina kazi kubwa sana katika kukupa muonekano mzuri wa ngozi ya mwili wako.Tunda hili husaidia kuboresha mzunguko wa damu mwilini pamoja na kuhifadhi ngozi isipoteze uhalisia wake.   PAPAI: Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa ngozi yenye mafuta, kurudishia au kuziba sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi yako. Papai pia hunga'arisha rangi ya ngozi yako, yote haya hufanyika na enzyme inayotokana papai ambayo huitwa papain. Endapo kama unataka kutumia papai katika ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya na papai lililo iva na paka usoni kwako kwa dakika 10 kisha safisha, kisha utaona kitakachotokea katika uso wako, utaonekana kama ngozi ya mtoto wa siku mbili.   AVOCADO: Tunda hili limekuwa maarufu sana kwa kutengenezewa juice, lakini huenda watu wakawa ha...