ZINGATIA HAYA KABLA NA BAABA YA KUOA
Kabla ya kuoa unapaswa kujiuliza maswali mengi na ukipata majibu ndio uamue kuoa,
kwanza jiulize kwa nini unaoa?
je umeandaa mazingira ya mke au umejiandaa kua mme?
ndugu zangu mabibi na mabwana, ndoa sio ngoma kua kila mtu anaweza kuicheza, ndoa ni kipindi kigum sana, ndoa ni kipindi cha mwisho cha maisha ya mwanadam, kipindi ambacho kinahitaji uvumilivu, unyenyekevu na uthamini wa mwenzi. siku hizi alie kwenye ndoa anatamani kutoka na ambae hajaingia anatamani kuingia, 😂😂😂😂 hiki ni kituko.
wakati huohuo wazinzi na waasherati wao kauli yao moja tu, BADO NIPO NIPO SANA,
wengine utawasikia wakisema "kama maziwa napata kuna haja gani ya kufuga ng'ombe?
Ndugu, marafiki, na jamaa, tambueni kua Ndoa ina umhimu mkubwa sana katika maisha ya mwanadam japo leo naongelea haya ambayo kama hutayazingatia daima utabaki kua mmiliki wa mkeo lakini dareva wa mkeo atakua mtu mwingine.................
siku zote anapaswa kujua kua mkeo alikubali umuoe kwa sababu anazozifahamu yeye japo upendo hua ni moja kati ya sababu hizo ingawa inaweza kutokea pia hata upendo ukawa haupo ila akakubali kuolewa.
lakini akisha olewa unapaswa kujua kua kuna vitu anapaswa kupewa na wewe kama mme na ikitokea ukaoa na ukashindwa kumpatia unapaswa kujiandaa kua mmiliki ila sio dereva wa mkeo.
gents and ladies..... chakula cha kutosha usiku ni mhimu sana katika ndoa yako na inapofika wakati wa chakula hiki wapaswa kukaza kamba ipasavyo, amini nakwambia ukilegeza utamegewa.
jiulize ni matajiri wangapi wanamegewa na wakata nyasi?
unafikiri kua ni u handsome au ni pesa?
ni ma sugar mammy wangapi wanamegwa na vijana?
ni kwa sababu wao wakipata nafasi wanaitendea haki, yaani wanajituma sana.........
Tafadhari hakikisha jambo hili unalifanya ipaswavyo na kama ukishindwa kumpatia tambua kua atalitafuta nje ya ndoa.
Kusema kweli nakushangaa sana wewe mwanamme unaeshinda ukila chips kuku, baga na mayai ya kizungu huku jioni ukinywa viroba ili kuongeza nguvu za kiume. hakika nakwambia ndoa yako itakua ndoano siyo mda,
kumbuka mapenzi yanahitaji maandalizi, kula vizuri, chakula chenye kuujenga mwili, kunywa maji ya kutosha na upate mda wa kupumzika......
unajisikiaje unapofunga goli moja then unahema kama bata wakati huo huo mwenzi wako akiwa hajafunga hata goli moja yaani unamaliza huku ukimuacha njia panda.......
hivi huoni aibu?
acha mapenzi ya kuku fikiria na uchukue hatua.......
MUDA.
jambo lingine ni muda.....
hakikisha mpenzi, mke au mchumba wako unampatia mda wa kukaa nae, siyo kila siku uko bize na biashara zako yaani wewe na pesa, pesa na wewe. inafika hatua ukirudi umechoka ni kulala tu, na ukiamka unawaza pesa, hebu fikiria ulikua na sababu gani ya kuoa na kuamua kulala nae kitanda kimoja.
mwenz wako anahitaji akae na wewe, azungumze na wewe na mpange mipango yenu pamoja, anapenda kujua changamoto unazokutana nazo kazini na mambo mengine pia, usidhani kwako alikuja kupika na kufua nguo zako, kumbuka alikuja ili mjenge maisha siyo kwa hayo unayoyafikiria wewe.
KUJALI.
Mwanamke siku zote anampenda mtu anaemjali, anaempenda na anaemsikiliza kila siku, anapenda mme wake awe imara siku zote, mcheshi na mwenye busara.
wewe kama mwanamme unapaswa kua katika hali hii....
mjali, mpende, mheshimu, mpe mda wako, mpe haki zake uone kama utasalitiwa na ikitokea ukasalitiwa basi tambua kua mwenzi wako ana kipaji cha umalaya au hakukupenda bali alikua nawe kwa sababu flani anazozijua yeye.
na utambue kua kama utashindwa kumfanyia mambo hayo siku ikitokea akampata anaejua manjonjo haya.....
basi wewe jiandae kuitwa mwanamme suruali, yaani wewe ni kasha lisilo na cd ndani.
MAZOEA
Kipengele hiki kimekua kikiwaponza wengi sana, unakuta mwanamme anamzoesha mwenzi wake, outing kila weekend, pombe, disco na mambo mengine ya kipuuzi, Naomba utambue kua siku ukiwa huwezi kumfanyia vitu hivi basi tambua kua utakua umemfungulia njia ya kukusaliti, mfano umesafiri mwezi mzima, unadhani hatatoka out? na wakati ulisha mzoesha.
hata kama atatoka na rafiki zako unadhani wote ni wema kwako?
kumbuka siku zote alipokua akilewa wewe uliangalia
Comments
Post a Comment