ZINGATIA HAYA KABLA NA BAABA YA KUOA Kabla ya kuoa unapaswa kujiuliza maswali mengi na ukipata majibu ndio uamue kuoa, kwanza jiulize kwa nini unaoa? je umeandaa mazingira ya mke au umejiandaa kua mme? ndugu zangu mabibi na mabwana, ndoa sio ngoma kua kila mtu anaweza kuicheza, ndoa ni kipindi kigum sana, ndoa ni kipindi cha mwisho cha maisha ya mwanadam, kipindi ambacho kinahitaji uvumilivu, unyenyekevu na uthamini wa mwenzi. siku hizi alie kwenye ndoa anatamani kutoka na ambae hajaingia anatamani kuingia, 😂😂😂😂 hiki ni kituko. wakati huohuo wazinzi na waasherati wao kauli yao moja tu, BADO NIPO NIPO SANA, wengine utawasikia wakisema "kama maziwa napata kuna haja gani ya kufuga ng'ombe? Ndugu, marafiki, na jamaa, tambueni kua Ndoa ina umhimu mkubwa sana katika maisha ya mwanadam japo leo naongelea haya ambayo kama hutayazingatia daima utabaki kua mmiliki wa mkeo lakini dareva wa mkeo atakua mtu mwingine................. ...