Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2016

BILIONEA AMZIKA MAMA YAKE NDANI YA GARI(HAMMER)

BILIONEA WA KINIGERIA AMZIKA MAMA YAKE NDANI YA HAMMER BADALA YA SANDUKU Check picha

FAHAMU FAIDA ZA KUJAMBA

Ni kama mzaha lakini uchunguzi wa kisayansi unaonesha hivo. Watalaam wamegundua kujamba kuna faida za kupunguza uwezekano wa kupata saratani na shambulio la moyo vile vile kunusa halufu ya mtu aliyejamba inasaidia ubongo kufanya kazi vizuri na kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa Dementia... Tujambe jamani kuboresha afya zetu

UTOFAUTI WA KUTUMIA MUDA NA UTAJIRI

DONGO LA PESA NA MUDA....... Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda.. -Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa kuliko ya basi, why..? Because ndege hutumia mda mchache (mf. Ukitoma dar kwenda moshi ni dk45 tu kwa ndege bt kwa gari ni takriban masaa 7-8) *Linapokuja suala la MUDA NA PESA, duniani kuna makundi manne ya watu...! 1. wapo wenye muda wa kutosha bt hawana pesa mf watu wasio na kazi maalum au wa kijiweni(ukimwambia akusindikize mahali yuko tayari muda wowote) 2. wapo wenye pesa lakini hawana muda. Unaweza kumualika ktk harusi akaacha kuja lakini akakuchangia hela ya maana tu.. hili ni kundi la madirector na mameneja wa vitengo muhimu ktk makampuni (ndio hawa JPM amewataka walipwe sio zaidi ya 15mil kwa sasa) 3. wapo wasio na PESA wala MUDA.. takwimu zinaonyesha kuwa hawa ni 95% ya watu wote ulimwenguni. Hili ni kundi la wafanyakazi na vibarua ( unaweza ukamualika ktk shughuli yako na akakosa nafasi lakini pia hana hela ya kukuchangia) Yaani mtu yuko busy 24/7 b...

MTOTO WA AJABU DUNIANI KAZALIWA

Mwanamke mmoja nchini India amejifungua mtoto wa uzani wa kilo 6.8 ambaye madaktari wanasema huenda akawa mtoto mwenye uzani wa juu zaidi kuwahi kuzaliwa nchini humo. Mtoto huyo ana uzani sawa na mtoto wa umri wa miezi sita. Nchini humo, watoto huzaliwa na uzani wa kadiri wa kilo 2.5-3.5. Mamake Nandini, 20, alijifungua kupitia upasuaji katika jimbo la Karnataka, kusini mwa nchi hiyo. Afisa wa afya wa hospitali ya wilaya ya Hassan, Dkt Venkatesh R, amesema kwamba mtoto huyo pia ni mrefu wa kimo. Mtoto huyo ana kimo cha sentimeta 62 (inchi 24.4in) ilhali kwa kawaida watoto India huzaliwa na kimo cha sentimeta 50,"amesema Dkt SR Kumar, anayemtunza Nandini na mwanawe. Visa vya watoto kuzaliwa na uzani wa juu kupindukia sana hutokana na mama kuugua kisukari lakini madaktari wamebaini Nandini hana tatizo hilo. Rekodi ya mtoto mwenye uzani wa juu zaidi India inashikiliwa na mvulana aliyezaliwa na Firdous Khatun jimbo la Uttar Pradesh Novemba 2015. Mvulana huyo alikuwa na uzani w...

MADHARA YA ZINAA KISAYANSI

*MADHARA YA ZINAA KISAYANSI* Wengi katika wanadamu wanajaribu kuhoji kwa nini Allah anakataza zinaa wakati kuingiliana baina ya mke na mume na kuingiliana baina ya hawara na hawara mambo ni yale yale, sasa kwa nini akataze??? Kwanza ifahamike kwamba Allah akikataza jambo basi ujue lina hasara kwetu kwa kulifuata na lina faida kubwa kama tukiliacha. Tofauti na wanadamu, kwa mfano; Serikali inakataza pombe ya Gongo kwa madai kuwa ni haramu wakati Bia pia ni pombe lakini ni halali! Hiyo ni kwa mujibu wa serikali za ulimwengu. Lakini katika UISLAMU Mwenyezi Mungu akisema pombe ni haramu basi iwe Gongo,Bia,n.k zote ni HARAMU. Ndivyo pia ilivyo ZINAA, leo ulimwenguni kuna zinaa ya halali wenyewe wanaita “zinaa salama ya kutumia Condom” lakini uislamu umeharamisha kabisa zinaa, iwe ya Condom au bila Condom huo ndio uislamu na ndiyo amri za Allah. Allah anasema katika Qur’an, sura ya 17 Bani Israil aya ya 32; "Na wala msiikaribie ZINAA, hakika ya hiyo zinaa ni ...

MAMBO AMBAYO KIJANA HUTAKIWI KUYAFANYA…

(1). Kuchagua Kazi. Ni vigumu kupata Kazi ukiwa nje ya Kazi. Fanya Kazi uliyoipata upate Kazi unayoitaka. (2). Kuchagua sehemu ya kuishi /kufanyia Kazi. Maisha ni safari ndefu, maisha ni popote, si lazima kukaa mjini. Hauwezi kujua ni sehemu gan iliyobeba mafanikio yako. Chagua sehemu yenye FURSA na si yenye  MAGHOROFA. (3). Kuishi bila kuwa na malengo. Maisha si bahat mbaya au nzuri. Maisha ni mipango, Maisha yanaongozwa na malengo. Vile ulivyo leo ni matokeo ya jinsi  ulivyopanga jana, na vile unavyoishi leo ndivyo kesho yako itakavyokuwa. PANGA KESHO YAKO SASA. (4). Maisha Ya kuiga. Maisha yako si ya mwenzako, na ya maisha ya mwenzako si ya kwako. Si kila ukionacho ni lazima ufanye, chagua kipi cha kufanya na kipi cha kuacha. Kupitwa na jambo wakat mwingine sio USHAMBA ni BUSARA. (5). Kuishi juu ya kipato chako. Ishi kulingana na vile ulivyonavyo na si usivyonavyo. Kuwa na Busara katika MATUMIZI uepukane na MADENI yasiyo na ULAZIMA. RIDHIKA NA VILE ULIVYONAVYO. ...

FAHAMU JINSI YA KUFANIKIWA KIMAISHA

Kisaikolojia na kimaumbile binadamu wote ni sawa ila tunatofautiana jinsia na matumizi ya vitu tulivyopewa na mwenyezi Mungu. Na hii ndio hupelekea tofauti kubwa kati ya walichonacho (Matajiri) na wasionacho (maskini). Katika kuanza na ulichonacho leo tunaangalia vitu sita ambavyo tumepewa kama zawadi na Mungu. Na kila mtu amepewa sawasawa na mwenzie ila tofauti ni matumizi yetu katika kutupatia kile tunachokitaka katika maisha yetu ambacho ni Mafanikio. Ili kufanikiwa haijalishi upo katika hali gani, kitu kikubwa kwako ANZA NA ULICHONACHO KUPATA MAFANIKIO. Unaweza ukajiuliza kivipi? Usipate tabu. Ungana nami mzee wa Boda to Boda nikuhabarishe na kukupa nondo za kukuzindua katika usingizi ili upate mafanikio ya kweli. 1. AKILI. Ni ukweli kila binadamu ana akili ya kung'amua jema na baya ila sio wote wanaojua thamani ya akili walizonazo. Wapo wanazitumia kwa faida na malengo na kupata mafanikio ila wapo wanaozitumia vibaya na kuishia kuishi maisha ya shida hadi wanakufa. Ktk k...

ZIJUE SIRI MUHIMU KABLA YA NDOA

NI VEMA UKAYAJUA HAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA: 1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa ni ya maisha yote. 2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada ya Ndoa. 3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema. 4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi fanywa na mtu yeyote. 5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu. 6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama kuolewa na mtu asiye sahihi. 7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa: (a) Walevi (b) Wazinzi (c) Wagomvi. Aina tano za wanawake wa kuepukwa;    (a) Walevi    (b) Wazinzi    (c) Wachawi    (d) Wagomvi    (e) wasio tii 8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe na Ndoa yenye furaha. 9. Maneno matatu yanayojenga amani katika Ndoa: (a) Nakupenda. (b) Samahani. (c) Asante. 10. Kupiga punyeto kwa mwanaume na kujichua k...

FAHAMU TABIA ZA MWANAMKE MWENYE PENZI LA DHATI

MWANAMKE AKIPENDA ANAPENDA KWELI💑👫❤ Mwanamke akikupenda anakuwa na furaha, anakuwa anajivunia kuwa na wewe, na hujihisi furaha kuongea na wewe. Hupenda awe rafiki wa rafiki zako na ndugu zako, uvipendavyo na yeye atavipenda, atabadilisha mtindo wake wa maisha kuendana na mtindo wako. Haitajalisha ni kiasi gani utamuudhi, atakusamehe hata kabla hujamuomba msamaha, atachokifanya ni kusubiri tu umuombe msamaha kuthibitisha kama kweli umejutia kosa lako. Atajaribu kuwa na wivu na atakulinda kwani atahitaji uwe wake, wake peke yake na sio ku share. Atawakataa wengine wote wanaomtongoza kwa sababu ameona kesho yake ipo mikononi mwako. Haitajalisha ni kiasi gani uko mbali na yeye, atajilinda kwa ajili yako. Atalike na ku comment kila kitu unachoweka facebook hata kama ni cha kipuuzi (hahaahaa). Atakujibu kwa wakati text zako either watsapp, za kawaida au inbox ya fb. Hatajali kama unampa pesa au laa, kama ni tajiri au laa kwa sababu lengo lake ni kujenga maisha n...

ZIFAHAMU SABABU ZA KULIVUA PENDO

WAPENDAO NA WAPENDE Aah!! Moyo nchi ya kiza,, wewe pofu waendaje?? Mji hisia fukiza,, mwenzangu umechotaje?? mimi zimenitatiza,, machozi yanitokaje?? MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE Aah!! Nanena haya kwa ndani,, uwongo nitasemaje?? Utamu huo kinywani,, mapenzi umekaaje?? Niloipata tufani,, mapenzi yameumbwaje?? MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE Dah!! moyo unanisimanga,, maumivu yakataje?? Haya hayana nyakanga,, mwalimu kaumiaje?? Shetani nyumba kapanga,, wazimu kaingiaje?? MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE Doh!! sisemi naweka shonde,, waja mpate bwabwaje nafsi yangu ni kibonde,, utamu ningepataje?? Mbio nakwepa makonde,, na nyie mlitakaje?? MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE Dah!! Raha ya kuendeleza,, mwendo umepunguaje japo nisema naweza,, mawazo nikapambaje kumbe huitaji pweza,, mchuzi nitaunywaje MIMI NALIVUA PENDO,, WAPENDAO NA WAPENDE Duh!! Kukuru moyo kakara,, vuta vuta ngekujaje?? Mwili utake mitara,, nafsi nimechafukwaje?? Pen...

SIRI KUBWA KUFANIKIWA MAISHA KABLA YA MIAKA 40

Kuna makundi manne (4) ya watu wanaotengeneza pesa hapa duniani. 1. WAAJIRIWA. Hawa ni watu ambao kimsingi wanauza muda wao almost wote wa siku nzima kwa mwajiri wao na yeye anawalipa pesa kwa kuwaambia cha kumfanyia. Kwa kuwa kanuni ya mshahara huwa ni kumlipa mtu 10% ya anachozalisha hasa kwa makampuni makubwa basi haitakaa itokee mwajiriwa kulingana kipato na mwajiri wake. Na hivyo wengi wa waajiriwa hufa #maskini na watoto wao pia kuanza kutafuta maisha kivyaovyao kwa kusoma na kuja #kuajiriwa pia hivyo hivyo.. Usikubali kubaki kwenye ajira unalipwa laki 5 kwa mwezi sawa na Tsh 1,850 yaani chini ya dola moja kwa saa. Ina maana umesoma mpaka chuo kikuu halafu thamani ya lisaa lako moja ni less than $1!!!!? Ndiyo maana watu wengi waliosoma sana huwa hawawezi kuwa matajiri kwa sababu wanauza muda wao kwa "bei chee" halafu siku zinazidi kuyoyoma haoni mafanikio. Huku tena ana mkopo wa gari nk. Makato na marejesho... Kwa nini usife masikini kwa style hiyo.? 2. WALIOJIAJIR...

MAJINA YOTE YA KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA JKT 2016

Bonyeza hapa kuona kambi pamoja na majina yote ya vijana wa kidato cha sita 2016 waliopangiwa jkt kwa mujibu wa sheria http://jkt.mil.tz/vikosi-walivyopangiwa-wanafunzi.html

JINSI YA KUPATA UTAJIRI KWA KUTUMIA AKILI YAKO

AKILI YAKO UTAJIRI WAKO: Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU . Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji. Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza. Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza! Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zika...

SIFA ZA BANDA BORA LA KUKU

Sifa za #Banda Bora la #Kuku 1. Ukubwa wa banda ulingane na idadi ya kuku ( 1m square wakae kuku 4) 2. Hewa na mwanga wa kutosha 3. Paa limwezeshe mtu kuingia ndani akiwa amesimama na kufanya usafi 4. Lisiingize maji ya mvua 5. Lizuie maadui kuingia (paka, mwizi n.k) 6. Sakafu isiyotuamisha maji 7. Ongezea nyingine tubadilishane mawazo

MBINU 5 ZA MAFANIKIO KIUCHUMI

Mbinu 5 Muhimu Za kukupa Maisha Ya Mafanikio. Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa  ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanini nyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu Fulani kufanikiwa. Kawaida, katika maisha kama ulivyomchezo wa miguu, au michezo mingine mara nyingi huwa zipo mbinu za kufanikisha kile tunachokifanya. Mbinu hizi huweza kutambulika kama sheria, kanuni, au siri lakini zote hulenga kukufanikisha kama unataka mafanikio ya kweli. Mbinu hizi zinapotumiwa kwa bahati mbaya au nzuri huwa hazifanyi ubaguzi zinamwendea yoyote na kuleta matunda unayoyataka...

FAHAMU MAMBO 20 YA AIBU AFANYAYO MWANAUME

AIBU 20 ZA WANAUME: 1. Japo maisha ni kusaidiana ni aibu na fedheha mwanaume kulishwa na mkewe.🙈 2. Ni aibu na fedheha mwanaume kuhamia kwenye nyumba ya mkeo ukakala ukakoroma na taulo ukafunga..🙈 3. Ni aibu na fedheha kuendesha gari la mkeo wakati wewe hujawahi kumiliki gari alafu unawaka wivu juu yake.🙈 4. Ni aibu na fedheha kuishi na mwanamke ambaye wakwe zako wanajua kuwa anakuzidi uwezo.🙈 5. Ni aibu na fedheha kumuoa mwanamke ambaye anamiliki uchumi wa familia hata watoto anasomesha yeye wewe unajivunia uume mkubwa au urefu wa kimo🙈 6. Ni aibu na fedheha kila likizo unaenda kijijini kwa mkeo na watoto wote kisa yeye anazohela🙈 7. Ni aibu na fedheha kukaa miaka mingi unamlaumu mkeo kuwa hazai wakati wewe huna hata mtoto wa kusingiziwa🙈 8. Ni aibu na fedheha kumrudia mwanamke aliye kuacha yeye mwenyewe kipindi kirefu na akaamua kukurudia yeye mwenyewe tena kwa masharti kutoka kwake.&#1285...

JINSI YA KUJENGA NDOA BORA

NDOA ni shule pekee ambayo unapata cheti kabla ya kuanza masomo. Ni shule ambayo kamwe hauwezi kuhitimu. Ni shule ambayo unatakiwa kuhudhuria siku zote za uhai wako. Ni shule ambayo hakuna likizo ya kuumwa au sikukuu. Ni shule ambayo iligunduliwa na Mungu katika misingi ifuatayo; 1. Msingi wa upendo. 2. Kuta za shule zimejengwa kwa "uaminifu" 3. Madirisha yametengenezwa kwa "uvumilivu" 4. Samani zimetengenezwa kwa "msamaha" 5. Na ikaizekwa kwa "Imani" Ukumbuke kuwa wewe ni mwanafunzi tu na sio mkuu wa shule ya NDOA. Mungu ndio Mkuu wa Shule. Hata wakati wa mapito, majaribu, kimbunga na misukosuko ya hapa na pale usikimbie nje ya shule. Kamwe usiende kulala kabla hujamaliza homework yako. Kamwe usisahau kusoma somo la mawasiliano. Wasiliana na mwanafunzi mwenzio pamoja na Mwalimu mkuu. Kama utaona kuna kitu kwa mwanafunzi mwenzako ambacho kimsingi haukipendi, basi ukumbuke mwenzako nae ni mwanafunzi na sio mhitimu mwalimu Mkuu bado haja...

VUNJA MBAVU

Baba: Unampenda nani zaidi kati yangu mimi na mama yako? Mtoto: Nawapenda wote. Baba: Kama nikienda Marekani na mama yako akaenda Paris, wewe ukaambiwa umfuate mmoja utaenda wapi? Mtoto: Paris. Baba: Okay kwahiyo unampenda zaidi mama yako, sio? Mtoto: Hapana, kwa sababu naipenda zaidi Paris. Baba: Okay, na mimi nikienda Paris na mama yako akaenda Marekani wewe utaenda wapi? Mtoto: Nitaenda Marekani. Baba: [kwa hasira] Kwanini wakati umesema unapenda zaidi Paris? Mtoto: Kwa sababu nitakua tayari nimeshaenda Paris. Baba: Pumbavu, umeenda lini Paris. Mtoto: Kwenye swali la kwanza ulilouliza.! 😂😂😂